Jurgen Klopp amekubali kandarasi ya miaka mitatu kuwa mkufunzi wa kilabu ya Liverpool.
Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 48 anachukua mahala pake Brendan Rodgers ambaye alifutwa kazi siku ya jumapili baada ya kuiongoza timu hiyo ambayo iko nafasi ya 10 katika jedwali la ligi ya Uingereza kwa miaka mitatu na nusu
Anatarajiwa kumleta Zeljko Buvac na Peter Krawietz,manaibu wake wa zamani katika kilabu hiyo ya Bundesliga ili kujaza safu yake ya ukufunzi.
0 comments:
Post a Comment