JE KUNA MBINU MBADALA KWA BENITEZ?

Mechi ya Real Madrid dhidi ya  Atlético Madrid iliendele kumuelezea Rafa Benítez kwa sifa yake ya kuwa kocha anayependelea kucheza kwa kujihami.
Mbinu zake alizotumia kwenye mchezo huo uliochezwa pale Vicente Calderon zimepelekea kuzuka kwa wasiwasi kwamba ni kweli yeye ndio mtu sahihi wa kuipa timu maisha mpya.


 LBenitez aliwasili Bernabeu akiwa na umaarufu wa kuwa kocha anayepnda kucheza kwa kujihami zaidi na sifa hiyo bado ameendelea nayo na inaishi katika kikosi chake cha Real Madrid – lakini baada ya ‘derby’ ya wikiendi iliyoisha maswali yameanza kuwa mengi.
Wachezaji wake nao wamezidi kuongeza juzi kwenye kidonda kipya: “Alikitoa nje kwa sababu ya ubao wa matokeo, alihitaji kuzuia zaidi ili kulinda goli”, alisema Benzema kuhusiana na kutolewa na kocha katika kipindi cha pili.
Ni wazi kwamba kipaumbele cha kwanza cha Benitez wakati akiwasili BernBeu ilikuwa ni kujenga safu ya ulinzi imara na rekodi ya Madrid msimu huu inaonyesha lengo lake linatimia, wakiwa wameruhusu wavu wao kuguswa mara 2 tu.
Japokuwa, kuna baadhi ya wadau wanaonyesha kwamba mafanikio hayo yanatokana na ubora wa juu ya golikipa Jesus Navas na mfano mzuri mechi iliyopita dhidi ya Atlético.
Ni muda tu utakaongea juu ya mbinu za Benitez, je ana mbinu mbadala, mpaka sasa Real Madrid wameshafunga magoli 15 katika mechi 7 za La Liga na sita kati ya hayo yamefungw dhidi ya timu moja – Espanyol.

0 comments:

Post a Comment