BARNABA AMEONESHA KIONJO CHA WIMBO WAKE WA "NAKUTUNZA"

Barnaba classic ameachia kionjo cha wimbo wake mpya aliofanya na msanii kutoka Uganda, Jose Chameleone, wimbo ambao umepewa jina la Nakutunza.

Ngoma hii ilibidi itolewe leo ila kutokana na mambo ya uchaguzi, Barnaba na uongozi wake ukaamua kuachia ngoma hii Alhamisi ya wiki ijayo

Barnaba aliandika katika kurasa yake ya Intagram  tarehe rasmi ya ngoma yake hiyo
Heloooo #Tanzania hello. Wapendwa na mashabiki Zangu !ambao Wote Najua Mlikuwa Mkisubiri Kwa Hamu wimbo wa #Nakutunza !!/ Sasa kutokana na Kaz Ya Uchaguzi Mkuu wa Jamuhuri Ya muungano Wa Tanzania Nisingeweza Kutoa wimbo Leo mana Bado watu walikuwa wa kimsubiri kiongozi Ambaye Ataliongoza Taifa na maslai Ya watanzania kwa Ujumla Ivyo Bass napenda Kusema Tunawaomba Radhi Na Tumesogeza Kutoka Leo 30/October Mbaka Tarehe 5/-November Itakuwa Alhamisi’ na Kutokana na mambo Ya kitaifa Tumeheshimu Uchaguzi!!.. na Kwa heshima na Busara Tumeamua mbaka kiongozi wetu Atakapoapishwa na kupata Baraka ya Nchi Nasi tutaendelea sasa kwaiyo Nomba Sana kwa Watu wa #midia mbali … Na hata mashabiki zetu wa sehemu mbali mbali mana Tumekatili Mioyo Yenu ….!! but Tukutane 5/-November lakini Leo nitaweka Baadae Sekunde 15 Za Chorus Au Kiitikio ambacho Barnaba ameimba na @jchameleone na Sehemu ambayo Barnaba ameimba #kiganda Kidogo Maneno Ya wimbo mbaka Apo Alhamisi Mwambie mwenzako au #Tag mshikaji au Repost kwa Kuonesha love na upendo Ili Tusogeze muziki wetu mbali Asanteni Sana” Aliandika barnaba.

0 comments:

Post a Comment