BAADA YA KUPIGWA KOTE NA CHRIS BROWN RIHHANA ALISEMA KWAMBA ANGEWEZA KUMBADILI CHRISH

H
Siku chache zilizopita Rihanna alifanya interview na gazeti la Vanity Fair, la Marekani na kuzungumza vitu vingi ikiwemo mahusiano yake ya zamani na R&B superstaa Chris Brown.
Baada ya kujibu maswali mengine yote, maswali juu ya yeye na aliewahi kuwa mpenzi wake Chris Brown yalifuata… kwenye kuzungumza Rihanna alisema kuwa licha ya yote yaliokuwa yanatokea kati yake na Chris Brown staa huyo bado alikuwa anajaribu kulinda hisia alizokuwa nazo juu yake lakini sasa hivi hana uhusiano wa aina wowote ule na Chris Brown ila bado anamjali sana staa huyo…
>>> “Nilikuwa najaribu sana kumlinda Chris, yeye pamoja na hisia zangu juu yake… mara nyingi nilikuwa nahisi watu hawamuelewi, hata baada ya ile issue kutokea na watu kuongea… lakini unajua inakuwa ngumu ya wewe kuona picha halisi ya mtu na jinsi mambo yalivyo kama bado umekumbatia baadhi ya vitu fulani, haswa ukiwa bado unahitaji the best kutoka kwa mtu husika, na ukiwakumbusha makosa yao, au ukiyakumbuka yale matukio yaliokuumiza maishani, au hata ukijaribu kuonyesha kuwa upo tayari kuvumilia kitu au mtu, wataishia kukufikiria vibaya na kukushusha hadhi...<<< Rihanna.
>>> “… na ukijaribu kuvumilia, labda kwasababu unajaribu kujiridhisha kuwa pengine hiki ndicho [unachokistahili na kukihitaji] sasa hapo ndipo unapoanza kugundua kuwa ‘mmmh’ nilikuwa mjinga kuamini kitu hiki kinanifaa. Sometimes maamuzi sahihi na salama ni kuachana na hicho kitu… simchukii, namjali sana na nitaendelea kumjali mpaka siku nitakayokufa… ila tu mimi na Chris sio marafiki na sio kwamba mimi na yeye ni maadui pia. Imetokea tu hatuna uhusiano wowote sasahivi.” <<< Rihanna.

0 comments:

Post a Comment