Mvulana wa umri wa miaka 14 nchini Marekani, aliyegonga vichwa vya habari baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, amekutana na Rais wa Sudan Omar al-Bashir.
Ahmed Mohamed na familia yake walilakiwa katika ikulu ya rais katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum Jumatano
Kijana huyo ambaye alitengeneza saa ambayo ilimfanya apigwe pingu pindi alipoipeleka darasani kumwonesha mwalimu wake, ndipo hapo alipojizolea umaarufu wa kuwa ni kijana ambaye anaweza kujifunza vitu.
Safari yake hiyo ilimfanya kukutana na watu mashuhuri kama Raisi wa Marekani Barack Obama, CEO wa kampuni ya mtandao wa kijamii facebook na kuzawadia vitu kemkem kutoka Microsoft ambavyo vitamsaidia katika kujiendeleza kutengeneza vitu vingi zaidi
0 comments:
Post a Comment