Christiano Ronaldo anaweza kupata mshituko wa moyo akisikia jambo hili kuwa linataraji kufika mwisho.
Mwisho wa Ballon d’Or unakaribia kuisha Baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na Shirikisho la Soka la Ufaransa-FFF kumaliza mkataba wao.
FIFA Ballon d’Or ilitambulishwa mwaka 2010 kama jina rasmi la tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia kufuatia makubaliano na FFF. Hata hivyo, tuzo za mwaka huu zinaweza kuwa za mwisho za aina yake kufuatia Ufaransa kuchukua umiliki wa jina lao na kuhamisha mji mwenyeji kutoka Zurich.
Kumalizika kwa mkataba huo kunamaanisha kuwa sasa tuzo hizo zitatumia jina lake halisi la Mchezaji bora wa Dunia huku rais wa FIFA Gianni Infantinho na maofisa wengine wakijaribu kutafuta jina muafaka kwa ajili ya sherehe hizo. Kutokana na hilo, FIFA imesema inaangalia uwezekano wa kuhamisha tukio hilo katika miji tofauti kila mwaka
0 comments:
Post a Comment