UNAFAHAMU KWAMBA SIMU ZA ANDROID ZINAHIFADHI KILA KITU UNACHOFANYA?

Simu za Android zimekuwa ni miongoni mwa simu pendwa zaidi Duniani, lakini unafahamu kwamba hizi simu za android zinahifadhi kila kitu unachofanya kwenye simu yako?


Google ni kampuni pana ambayo unaweza kuikuta kila kona ya dunia ikiwa na lugha tofautitofauti, lakini kampuni hiyohiyo ambayo tunatumia kutafuta vitu huwa inahifadhi taarifa ya vitu tunavyotafuta mtandaoni, video unazoangalia youtube, apps ambazo unadownload playstore na vitu vingi.

GOOGLE INAHIFADHI VIPI KUMBUKUMBU ZAKO?
Inahifadhi kumbukumbu zako pale ulipoanza kujisajili kwenye Gmail na kwale ambao wanatumia simu za Android kumbukumbu zao huhifadhiwa pale wanapotengeneza account kwa ajili ya simu yako.


UNAONAJE KUMBUKUMBU ZAKO KWENYE GOOGLE?.
Ili kuweza kuona kumbukumbu za mambo yote ambayo umeyafanya katika Google tembelea website hii google.history.com 
baada ya kufunguka utaingiza email account yako kisha google itakuletea vitu vyote tangia mwanzo hadi mwisho.

0 comments:

Post a Comment