TANZANIA NJE MICHUANO YA AFCON
Timu ya Taifa Tanzania, Taifa stars imekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa timu ya Misri kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0, hivyo huu ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi kwa Taifa Stars, lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kutengeneza mazingira ya kufuzu AFCON 2017.
Kwa matokeo hayo Taifa Stars wanakuwa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.
PICHA:Millard ayo
0 comments:
Post a Comment