NEC IMEKABIDHI SHILINGI BILIONI 12 KWA RAISI MAGUFULI ZILIZOBAKI KWENYE UCHAGUZI MKUU MWAKA JANA



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imemkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh12bn zilizobaki baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka jana.

Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi hiyo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuokoa fedha hizo na kuzirejesha serikalini ili zipangiwe majukumu mengine na ametaka taasisi nyingine za serikali ziige mfano huo wa uzalendo na kutanguliza maslai ya taifa.

Rais Magufuli amelikubali ombi la tume kujengewa ofisi na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.

mlipewa zaidi ya Shilingi Bilioni 270, mkatumia shilingi Bilioni 261.6, mkabakiza shilingi Bilioni 12, mngeweza kuamua kusema hamkubakiza na hakuna mtu yeyote ambaye angewauliza, na saa nyingine pengine hakuna mtu yeyote ambaye angejua, mngeweza pia kusema kiasi mlichotupa hakijatosha, tunaomba mtuongezee ama mngetengeneze maneno mazuri mazuri ya matumizi, bado nina uhakika serikalini wasingejua” alisema Rais Magufuli.


0 comments:

Post a Comment