Kampuni ya mawasiliano nchini Tanzania Vodacom imezindua huduma ya mtandao wa 4G ambao utawawezesha watumiaji wa mtandao huo kufurahia huduma hiyo.
Uzinduzi wa Vodacom 4G umefanyika katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam huku uzinduzi huo ukisindikizwa na Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul makonda.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa spidi ya mtandao wa 4G wa Vodacom haina tofauti na ile inayopatikana kwenye nchi zilizoendelea.
Alisema kuwa mtandao huo utatumika kama chachu ya maendeleo kwenye sekta nyingi nchini.
“4G kwetu sio teknolojia, 4G kwetu ni kiwezeshaji, ni kiwezeshaji kwa serikali, kiwezeshaji kwa biashara, ni kiwezeshaji kwa watumiaji wetu,” alisema. “Inachofanya inafungua fursa mpya, uwezekano mpya,” aliongeza
mtandao wa 4G utarahisisha masuala muhimu kama mikutano inayofanyika kutumia mawasiliano ya video, ufanyaji masoko kwa njia ya kidijitali.
PICHA:BONGO5
0 comments:
Post a Comment