Tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) limetangaza majina ya filamu zitakazoshindanishwa hapo ifikapo Julai 9 hadi 17. Tamasha lilipokea jumla ya filamu 490 kutoka nchi 32 mwaka 2016.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo, Meneja wa Onyesho hilo, Daniel Nyalusi alisema, jopo la wachaguzi wa filamu limependekeza filamu 80 ndio zitakazoshindanishwa katika makundi matano maalum.
“Kundi la Kawaida 59, Sembene Ousmmane 15, filamu 12 Bongo movies. Nyingine 5 ni la kundi jipya kabisa la filamu zinazoizungumzia Zanzibar itakayopata tuzo ya Emerson,” alisema Daniel.
Alisem mwaka huu filamu za kitanzania zimeongezeka katika mashindano ambapo filamu 40 zilitumwa kwa mashindano kwa ujumla na mwaka huu filamu 5 za kitanzania zitashindanishwa katika jopo la Ousmane Sembene kati ya filamu 17.
Pia kwa ujumla filamu toka Afrika mashariki zilizoingia katika mashindano zimeongezeka pia ambapo kuna 8 toka Tanzania, Kenya 5, Uganda 3 na Rwanda 2.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Martin Mhando alisema mwaka huu kutakuwa na filamu 3 ambazo zitaoneshwa kwa mara ya kwanza duniani katika tamasha la ZIFF.
“Filamu hizi zimedhaminiwa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) wakishirikiana na ZIFF. Washindi watatu wa shindano la Sembene Ousmane mwaka 2015 walipewa $2000 kila mmoja kuwawezesha kutengeneza filamu mpya katika kipindi cha mwaka na kuzituma tena ZIFF kwa kushindanishwa na nyingine,” alisema Martin.
Pia alisema mvuto wa tamasha unazidi kukua kutokana na kuongezeka kwa nchi zinazotuma filamu. Ambapo mwaka huu Estonia na Albania zimetuma filamu zikiungana na nchi nyingine kama Bangladeshi, Finland, Trinidad and Tobago, Bermuda na nyinginezo.
ZIFF pia inaendeleza mchango wake katika tasnia ya filamu kwa kutayarisha warcha maalum juu ya utengenezaji filamu ambapo mwaka huu ZIFF imetangaza warsha mbili. Ya kwanza ni juu ya matumizi bora ya Camera ya Canon D5 itakayoendeshwa na Barry Braverman toka Marekani ,aliyeifanyia kazi Panasonic na Sony katika kujaribisha vifaa vyao.
Warsha nyingine ni ile itakayodhaminiwa na Goethe Institute ya Ujerumani itayofunza watoto wa shule ufundi wa kutengeneza vikaragosi katika filamu. Hii inatokana na kutambua nafasi ya sanaa katika kukuza vipaji na kuwatayarisha watoto wasanii kwa ajira, uadilifu na ubunifu.
0 comments:
Post a Comment