Rais John Magufuli ametoa salamu za pole kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza, kutokana na mauaji ya watu watatu, waliouawa kwa kukatwa mapanga wakiwa msikitini.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, jijini Dar es Salaam jana, ilisema Rais Magufuli amesema yupo pamoja na wakazi wa mkoa huo wa Mwanza katika kipindi hiki cha majonzi, kuomboleza watu hao na pia alisema anawaombea wale waliojeruhiwa wapone.
Serikali pia ilitoa pole kwa wakazi wa Mwanza na kusikitishwa na kitendo cha Mauaji jayo ya watu watatu jana katika Bunge kupitia Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Masauni Yussuf Masauni
0 comments:
Post a Comment