LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA KUENDELEA LEO



Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inaendelea leo katika hatua ya nusu fainali mchezo wa pili kati ya mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich dhidi ya Atletico Madrid kutoka nchini Hispania.

Atletico Madrid iliyoibuka na ushindi wa nyumbani wa bao 1-0 juma lilipita itakuwa na kibarua kigumu cha kukamilisha azima yake ya kutinga fainali kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu.
Bayern ili waingie fainal watakuwa na kibarua kigumu Zaidi cha kupindua matokeo ya mabao kwa kuwa wanahitajika kufunga mabao dhidi ya ukuta mgumu wa Atletico ya kocha Diego Simeone.

0 comments:

Post a Comment