KAMA WATOTO WADOGO WANGEKUWA NA SMARTPHONE ZAO MAALUMU INGEKUWA NI CHACHU YA UKUAJI ELIMU NA TEKNOLOJIA TANZANIA?
Wengi tumekutana na watoto wadogo wanaomiliki smartphone au kufunguliwa accounts katika mitandao ya kijamii, kwa mwanzo lilikuwa jambo la kushangaza nchini kwetu lakini Teknolojia inavyokuwa inaonekana ni jambo la kawaida.
Ulimwengu wa Teknolojia unavyokua nao unakuja na mambo mazuri ambayo yatafaa kwa mtoto vilevile na mambo mabaya ambayo hayafai kwa mtoto.
Watengenezaji wa Apps pia wamejitahidi kuweka Apps ambazo zitakuwa zikimsaidia mtoto kutumia simu kwa kujifunza vitu mbalimbali ambavyo ni kuchora, kuimba, kusoma, kupiga picha na hata kutengeneza application zao wenyewe.
Maoni kwa mawakala wa Kampuni za simu nchini pamoja na makampuni za mawasiliano nchini kuja na jambo la kutengeneza Smartphone ambazo zitakuwa maalumu kwa mtoto kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitaweza kuibua vipaji vingi nchini na kukuza Teknolojia nchini.
Kama ni sawa kwa mtoto kutengenezewa Smartphone yake mwenye weka comment yako hapa chini.
0 comments:
Post a Comment