GOOGLE WAMELETA HUDUMA MPYA KWA WATUMIAJI ANDROID NA IOS
Kampuni ya Google hivi karibuni ilifanya Kongamano lake linalowaunganisha developers mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani kwa ajili ya kutoa tuzo kwa watengenezaji bora wa application na uzinduzi wa teknolojia zingine kuhusu Android.
Kweneye kongamano la mwaka huu google i/o 2016 kampuni hiyo ilikuja na uzinduzi wa apps zake mbili ambazo ni ALLO na DUO zitakazo lahisisha ujumbe wa sms na video kuwa bora zaidi.
1:ALLO
Allo ni app mpya kabisa kutoka google ambayo inaweza kufanya mapinduzi na Whatsapp kutokana na sifa zao kuwa na ufanano. app hiyo ili kuitumia pia inahitajika namba ya rafiki yako kwenye simu lazima awe anatumia Allo ili kuweza kuwasiliana,
Pia allo imekujia na emoji mpya pamoja na google search ikiwa imo ndani ya App hiyo.
2:DUO
Duo ni app ambayo inakuja kuleta mapinduzi katika application za video call, duo inauwezo wa kufanya video hata mahala ambapo kuna network ndogo ya internet.
vilevile duo inakuja na uwezo wa kumwona anayekupigia hata kabla ya kupokea video call hiyo. app hii itakuwa kote kwa watumiaji wa Android na Iphone.
0 comments:
Post a Comment