Klabu ya Simba imepewa siku 30 na shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA kumlipa mchezaji wao wa zamani Donald Musoti
Fifa ilituma barua leo May 6 2016 kwa klabu ya simba na nakala kwa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, ambapo barua hiyo inataka klabu ya simba kumlipa Musoti fedha ya sh Milioni 64.2 pamoja na gharama ya idara ya kikao cha utatuzi wa migogoro.
Kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo. Kama Simba itashindwa kulipa deni hilo ndani ya siku 30, itaponywa point tatu au kushushwa daraja.
Musoti alifikisha malalamiko hayo kwa shirikisho hilo la soka Duniani FIFA kwa kumtumia mwanasheria wake Felix Majani.
0 comments:
Post a Comment