TUNZA UFANISI WA BETRI YAKO KWA KUACHA KUFANYA VITU HIVI
Teknolojia inazidi kupanuka na kila mtanzania sasa anamiliki Smartphone haijalishi ni yenye majina makubwa au hata yenye majina madogo, lakini kilio kikubwa cha watumiaji wa Smartphone ni chaji kutokaa kwa muda mrefu katika simu zao.
Kipi kinachosababisha chaji kuisha haraka? ni matumizi ya simu, betri mbovu au simu yenyewe? tuweke kando hayo ili nikupe sababu kubwa ambazo zinaweza kuwa ni chachu ya betri yako kuisha kwa haraka au kutokukaa na chaji kwa muda mrefu.
1:KUACHA SIMU KATIKA CHAJA USIKU MZIMA INAHARIBU UFANISI WA BETRI
Kuacha simu katika chaja kwa muda mrefu ni jambo ambalo linaweza leta maafa katika simu yako kutokana na Betri nyingi za smartphone huwa zinatumia lithium ion ambazo zenyewe ukiziacha kwa muda mrefu zinapata moto,ufanisi wa betri kupungua, kuungua na hata mda mwingine kulipuka kabisa.
2:KUCHOMOA SIMU KWENYE CHAJA KABLA YA KUJAA
Kuchomoa simu katika chaji kabla betri halijawa kamili ni tatizo pia kwani unakuwa unalipa wakati mgumu Betri lako kukumbuka asilimia ya chaji ambayo inahitajika katika simu yako, mfano kilaa ikifika asilimia 80 huwa unaichomoa hapo inakuwa inakariri na kufanya simu yako kuwa inajaza mwisho asilimia 80 tu.
3:KILA SIKU TUMIA CHAJI AMBAYO NI SAHIHI KWA KAMPUNI YAKO YA SIMU
Kutumia chaji ya simu ambayo imetengezwa na kampuni ya simu iliyotoka ni vizuri zaidi kuliko hizi zingine ambazo ni za bei rahisi kwani zinaweza hatarisha maisha ya betri yako
4:USITUMIE SIMU YAKO HUKU UNAICHAJI
4:USIPENDE KUTUMIA APPS KILLER
Usitumie kabisa hizo application ni uongo mtupu bali zinazidisha kutokufanya kazi kwa Betri yako.
Haya ni moja ya njia ambazo zinaaweza saidia kutunza kifaa chako betri yako bila kuisha kwa urahisi, kama una njia nyingine ambayo unaifahamu tupia comments yako
0 comments:
Post a Comment