RAISI MAGUFULI AMEVUNJA BODI YA TCRA KWA KUPOTEZA MAPATO YA BILLIONI 400

Rais Magufuli

Rais  Magufuli ameivunja Bodi ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simbakutokana na kutosimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS) na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingibilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 April 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Simba 2

JOHN

0 comments:

Post a Comment