Mkuu wa Mkoa Paul Makonda jumamosi hii ya tarehe 30 april amezindua kampeni ya usafi ambayo yamefanyika katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam.
Jambo kubwa ambalo lilimsikitisha Paul maakonda lilikuwa ni idadi ndogo ya wasanii ambao walihudhuria kampeni hiyo aidha pia aliwapongeza wasanii ambao waliweza hudhuria kampeni hiyo.
“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hichi ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii wowote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.
“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala kila mtu,” aliongeza Makonda.
Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.
Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.
Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.
0 comments:
Post a Comment