MAGARI 5 YA TFF YASHIKIRIWA NA MAMLAKA YA MAPATO NCHINI T.R.A



Huku tetesi za kocha wa timu ya taifa,Taifa stars,Boniphace Mkwasa kutaka kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kutolipwa stahiki zake,mamlaka ya mapato nchini (TRA) kwa mara nyingine wameligeukia  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuyachukua  magari matano  yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kitita kikubwa cha kodi.
TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.
Richard Kayombo  afisa habari (TRA) amethibitisha kuchukuliwa kwa magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu za zilizopelekea kufanya hivyo.“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanatokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa.”alisema.
“Mpaka sasahivi tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, kodi hizo ni  VAT, pay as you earn na SBL,ila  ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu eni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”aliongeza Kayombo.
Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.
Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

0 comments:

Post a Comment