vijana wa kitanzania waliokuwa wakisoma nchini Marekani wamekuja na application ya kupata huduma ya usafiri kwa muda wote na popote ulipo ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Kundi hilo la vijana likiongozwa na Godwin Ngugulile, wameamua kuja na huduma hiyo kwa mara ya kwanza nchini Tanzania japo nchi kama Marekani tayari ilishaanza kutumika miaka mingi iliyopita na zingine bado zikiendelea kufanya vizuri baadhi ya nchi za Kimarekani miongoni mwa huduma hizo ni Uber
“Kwa huduma itakuwa ni masaa 24, kama dereva kwenye application yake ipo on unaweza uka mbuku dereva huyo na ukapata huduma hiyo ya usafiri,” alisema Ndugulile
Mpaka sasa vijana hao wameshaweza kuajiri zaidi ya vijana 8600 wakiwemo madereva tax, pikipiki na bajaji, kwa ajili ya kutoa huduma hiyo ya usafiri kwenye jiji la Dar es Salaam na bado kila siku wastani wa madereva 20 hadi 70 wanajitokeza kwa siku ili kujiunga kwenye mfumo huo wa kiteknolojia.
0 comments:
Post a Comment