FACEBOOK IMEKUJA NA MBINU MPYA KWA WATU WASIOONA



Huku mtandao ukitawaliwa na picha chungu nzima ,mtandao wa Facebook unazindua mbinu ambayo inaweza kuzisoma picha na kuwaelezea watu walio na ulemavu wa macho kile kilichomo katika picha hiyo.
Mtandao unabadilika. Badaya ya kuanza kwa kutumia maandishi sasa umebadilika na picha ndio kiungo muhimu.
Takriban picha milioni 1.8 huchapishwa katika mitandao kama vile Twitter,Instagram na Facebook.
Ni habari njema kwa wale wanaotaka kujiunga na upigaji picha na mbaya kwa walemavu wa macho ambao hawawezi kujua ipi ni picha licha ya kuwepo kwa teknolojia zinazoweza kuwasaidia.
Lakini huduma mpya kutoka facebook ,iliozinduliwa siku ya Jumanne inajaribu kukosoa hilo.Walio na ulemavu wa macho hutumia programu zinazoitwa Screenreaders ili kuweza kutumia Kompyuta.
Hubadilisha yaliomo ndani ya vioo vya vifaa hivyo kuweza kusikika.
Lakini wanaweza kusoma maandishi na wala sio picha.
Lakini kwa kutumia mfumo wa kuweza kufikiria ,wanaotoa huduma ya facebook wana uwezo kusoma na kuzielezea picha zilizopakuliwa katika mtandao huo na kuziweka katika hali ambayo zinaweza kusomwa na kifaa cha screenreader

0 comments:

Post a Comment