DARAJA LA KIGAMBONI LINATARAJIWA KUZINDULIWA RASMI NA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI LEO 19 APRIL 2016
Raisi John Pombe Magufuli anatarajiwa kufungua Daraja la Kigamboni leo na kuweka miundombinu ya usafiri wa kisasa Nchini.
Daraja la Kigamboni limejengwa kwa ushirikiano wa kampuni mbili za Ukandarasi ambazo ni CHINA RAILWAY MAJOR BRIDGE ENGINEERING(MBECL) na CHINA RAILWAY CONSTRUCTION ENGINEERING GROUP(CRCEG). Mradi huo ulichukua miaka 4 na kugharimu Sh.214.6 Bilioni zitokanazo na vyanzo vya ndani kwa ushirikiano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na wakala wa Barabara Tanroads.
Kwa sasa Daraja hilo linatumika Bure kwa wananchi wote mpka pale Mamlaka husika zitakapo kubaliana juu ya kuweka kiasi husika ambacho kitastahili kwa wananchi.
Urefu wa Daraja la Kigamboni ni mita 680 huku kitako cha daraja hilo kinashikiliwa na Nguzo ambazo zimezamishwa Baharini.
0 comments:
Post a Comment