Mwamuzi wa Kike wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuchezesha michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q17) mwisho wa mwezi huu.
Katika mchezo wa Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa jijini Cairo wikiend ya tarehe 25, 26, 27 march, Jonesia Rukyaa atakuwa mwamuzi wa akiba akiungana na waamuzi wengine kutoka Kenya kuchezesha mtanange huo.
0 comments:
Post a Comment