

Almasi masaond ni kijana ambae hivi sasa amejiandaa na ujio wa video yake mpya inayokwenda kwa jina la Baishoo, video ambayo imefanywa na Director Deo Abel chini ya uongozi wa Sweseka Production.
"Mziki ulikuwa unanafasi kubwa sana katika maisha yangu kuliko shule, kwasababu mziki mimi nilianza kuimba tangia nikiwa Form one huko kigoma" Alisema masound
Katika kipindi chake cha mziki, Almasi alishafanya ngoma tatu ambazo alizifanya alipokuwa Kigoma huku akipewa sapoti kubwa kutoka kwa Sentano records.
"Nilishafanya nyimbo tatu ambazo zilikuwa ni NIKUIMBIE, MY na NITUNZE hizi nilizifanya kupitia studio ya Sentano records pamoja na Grey bakuza records" Aliendelea masound
Almasi kwa sasa yupo chini ya Sweseka production ambao ni wamesimamia ujio wa ngoma na video ya Baishoo ambayo inategemewa kutoka hivi karibuni.
Santeee asanteeeeh
ReplyDeleteTunaisubir kwa hamu
ReplyDelete