APPLICATION NYINGI ZA BURE ZINAWEZA KUTUGHARIMU KATIKA SIMU ZETU, FAHAMU KWANINI


Wote tunapenda application za bure katika Smartphone zetu kweli? kwasababu tukiona app ambayo iko free kwa kudownload ndio tunaipa kipaumbele kubwa kutokana hainigharimu senti yeyote.

Habarika leo itakufahamisha kwanini kuna umuhimu muda mwingine kununua Application katika simu yako, najua vipato wengine viko chini ila hebu tujiulize kidogo...Kutengeneza Application ili sisi tuweze kuifurahia na kuitumia ni kazi ngumu sana pia huyo aliyeandaa hiyo app anaitaji kupata chochote kitu.

Baada aya uchunguzi wa mda mrefu kufanywa unaonesha kuwa Apps nyingi ambazo ni zabure zinaharibu mfumo endeshaji wa simu zetu kufanya kazi zaidi tunavyofikiri...unajua ikoje hapo? iko hivi.

1.MATANGAZO YANAKERA MDA MWINGINE.
Iko hivi unakuta umedownload App yako kama ni Game au kitu chochote kile, unajikuta ndani ya dakika 2 ya matumizi ya hiyo application linajitokeza tangazo, najua kila mtu anakereka na vitu hivyo
Screenshot_20160313-135843

2.MATANGAZO YANAUWA UFANISI WA BETRI YA SIMU.
Katika tafiti zilizofanywa na Chuo cha USC, UCSE na RIT wanasema kwamba App ambayo umeidownload alafu ndani inakuwa na matangazo huwa inapunguza asilimia 16% ya betri yako kwa masaa mawili na nusu.

Kila siku tunajaribu kuweka Betri zenye uwezo mkubwa au kununua simu ambazo zinakaa na Betri mda mrefu na kuweka Saving modes za kutosha kumbe umesahau kama una Apps kama 10 ambazo kila moja linatangazo na kila moja linamaliza Betri yako kila masaa mawili.

3.SMARTPHONE YAKO ITAANZA KUFANYA KAZI TARATIBU
Siku zote simu inapokuwa mpya huwa inakuwa inafanya kazi kwa haraka sana, ila siku kadri ya siku inaanza kufanya kazi taratibu hii inatokana na sababu nyingi kibao lakini mojawapo ni hizi Application za Bure zenye Matangazo kwasababu huwa zinachukua asilimia 48% ya RAM yako.


4.APPS NYINGI ZA FREE ZINAKUWA HAZINA UBORA.
Google-Play-Store-11
Tunarudi kulele hakuna mtu ambaye hapendi kuzawadia kitu pale anapofanya kazi nzuri, sasa unakuta Developer ametengeneza App yake na wala hata mpango wa kutunukiwa zawadi yeyote ile unafikiri hiyo App itakuwa inapata Updates kweli? Haiwezekani na ndio maana apps nyingi huwa hazina ubora.

Mwisho sina maana ya Apps zote za Bure ni mbaya zipo hata za kulipia nazo unakuta zinamatangazo kemkem cha msingi ni kuwa makini na Apps aambazo tunazidownload zisiwe na matangazo kwani ni chanzo ufanisi wa Simu zetu kupungua kufanya kazi zake.

0 comments:

Post a Comment