Katika ulimwengu wa sasa ukisema neno Apple kwa asilimia kubwa utaeleweka kuwa unaamanisha Kampuni na si tunda kutokana na bidhaa zake za Iphone, Ipad, Imac na Ipod kutawala ulimwengu.
Lakini ushawahi kuwaza au kufikiri kwanini Kampuni ya Apple inatumia neno "I" katika kila bidhaa yake? kuna maana yoyote juu ya hili? sasa maana ya kutumia neno I katika bidhaa ni hapa..
Kutumika kwa neno I kulianza mnamo wa mwaka 1997 pale CEO steave Jobs aliporudi katika kampuni yake ya Apple kutoka kwa Next Computers.
Steave Jobs na team yake wakafanikiwa kutengeneza Computer yao ya kwanza ambayo ilikuwa na uwezo wa kutumia (USB), 3.5 floppy disk drive pamoja na CD Rom drive na kuipa computer hiyo jina la "MACMAC", ilikuwa ngumu kwa team yake kukubali neno hilo la MACMAC mpka pale aliposema sababu ya kuanzisha computer hiyo
"It's a full-powered Mac, so it can do a lot of things. But first and foremost, it will get you onto the Internet in 10 minutes, even if you've never used a computer
before." alisema Steave Jobs
Hapo ndipo neno la I lilipotokea kwamba litasimama badala ya INTERNET kutokana na kipiondi hicho Computer hiyo ilikuwa na uwezo wa kukupeleka kwenye Internet ndani ya dakika 10, na kuipa jina la IMAC.
Hapo ndipo kampuni ya Apple kuanza kutumia neno I katika kila bidhaa zake kama iphone, ipad, ipod na Imac.
0 comments:
Post a Comment