WANAOTUMIA INTERNET EXPLORER MATOLEO YA ZAMANI WAKO HATARINI
Kampuni ya Micrososft imetangaza kuwa watumiaji wa Internet Explorer kuanzia 8, 9, 10 hawatopata Updates za Browser hiyo na kwahiyo kufanya Siri zao kuwa Hatarini kuvamiwa na Wadukuzi.
NetMarketShare inakadiria kwamba wanaotumia Internet Explorer mtandaoni ni 57% wakilinganishwa na 25% wanaotumia Chrome, 12% wanaotumia Firefox na 5% wanaotumia Safari.
"Kuanzia tarehe 12 january 2016 matoleo ya Internet Explorer kama 11 na Edge ndiyo yatapata Updates za Kiufundi zaidi na usalama" Micrososft wamesema
Kampuni ya Micrososft inawahimiza kuwa watumiaji wake wa Internet Explorer version ya zamani inabidi waanzze kutumia maboresho haya mapya kama Internet Explorer 11 na Edge
Kampuni hiyo inaendelea kutoa usaidizi kwa matoleo ya IE 11 na Edge, ambayo kimsingi ndiyo hutumiwa na Windows 10.
0 comments:
Post a Comment