Kupitia mtandao wa Habari wa BBC umeeleza kuwa kundi la wapiganaji wa al-Shabab liko huru kushiriki katika ligi kuu ya soka nchini humo.
Abdiqani Said Arab amemuambiwa mwandishi wa BBC jijini Nairobi John Nene kwamba iwapo wapiganaji hao wanataka kushiriki watepewa fursa.
''Hatuwapingi na hawatupingi," alisema.
Kundi la al-Shabab linaloendesha itikadi kali, limewaagiza wanasoka kuvaa suruali ndefu na limepiga marufuku muziki katika maeneo linalodhibiti.
Hata hivyo, Bw Arab amesema kuwa anaamini kwamba wafuasi wa kundi hilo wanahudhuria mechi za soka lakini akakataa kutoa maelezo zaidi.
Mwezi Uliopita,mechi moja nchini Somalia ilipeperushwa moja kwa moja katika runinga ya kitaifa kwa mara ya kwanza.
SOURCE:BBC-
0 comments:
Post a Comment