NICKI MINAJ AMETOA DOLA 100.000 KAMA DHAMANA KWA KAKA YAKE

Nick Minaj amemlipia dhamana kaka yake, Jelani Maraj (37) baada ya kukamatwa kwa mashitaka ya kubaka mtoto wa miaka 12.
Jelani Maraj aliachiwa Ijumaa iliyopitwa [Dec. 4] baada ya dada yake kulipa dhamana ya dolla 100,000, Kwa mujibu wa New York Post dhamana hiyo ni ya nyumba mbili za rapper huyo mwenye umri wa miaka 32, moja anakaa Mama yake na nyingine ilikuwa inatumiwa na Kaka yake.
Jelani alikamatwa Alhamisi ya wiki iliyopita kwa kosa la kulazimisha ngono (ubakaji) na kufanya mapenzi na binti wa miaka 12, Kila kosa lina adhabu ya kifungo cha miaka 25, hata hivyo bado haijatajwa lini kosa hilo lilitendeka.
Mwezi wa nane, Nick Minaj alitoa dolla 30,000 kwa ajili ya Harusi ya kaka yake huyo, Pia aliweka post yenye ujumbe unaosomeka
“I would cross the ocean for u. I would go & bring u the moon. Promise u. For u I will,” Aliandika “I love my brother so much man,’ she added. ‘I do anything to see my brothers smile.” Aliongeza.
Bila shaka Nick Minaj alimaanisha, Kesi hiyo itasikilizwa tena December 9.

0 comments:

Post a Comment