Watu hawa ndio walitajwa na Peter Msechu kuwa walimwambia uandishi wa nyimbo zake hauko vizuri na ndio waliokuwa wakimpa mapungufu ambayo yalikuwa yanamfanya kutofanya vizuri
Kupitia Amplifaya ya Clouds FM, Peter Msechu alimtaja Ruge Mutahaba, Master jay, Ditto na Barnaba ndio watu wa mwanzo kumpa ukweli juu ya uandishi huo ambao ulikuwa sio mzuri.
"Mtu wa kwanza kunipa ushauri alikuwa ni Ruge kwasababu alinita personally na kuniambia uwezo wa kuimba ninao ila njia ninayoenda sio, Ditto aliniita akaniambia kuwa Msechu unakosea, Ile ngoma ya Hasira hasara Master jay alinieleza vizuri tu, Richard horombe ambaye alikuwa meneja wangu, Tee jay alinifata akaniambai kuwa napiga kelele tu, Mwasiti Barnaba alishaniambia kuwa naimba vitu vingi ni calm down ni sipanic, kidumu, R kay na Kavutha alikuwa voice coach wa Tusker project fame aliniambia kuwa nimeachia ngoma yangu ila nina shout masikioni...kwahiyo watu hao walinisaidia sana" Alisema peter Msechu kupitia Amplifaya ya clouds fm.
0 comments:
Post a Comment