Umeshawahi kuwaza kuwa jinsi umbali wako wa kutembea kwa ndivyo unavyoingiza pesa?yani kila hatua moja unazalisha pesa?
Kupitia Mtandao wa Habari wa BBC umeeleza kuwa hivi sasa watu watakuwa wanalipwa kwa kila hatua wanazotembea kwa mwezi baada ya kujumlishwa hatua hizo.
Programu ya Bitwalking ni programu ambayo itakuwa inamlipa mtu kwa hatua zake anazotembea kwa mwez mzima, na pesa ambazo utakuwa unapata kupitia programu hiyo zitasaidia Mtumiaji kununua bidhaa Mtandaoni(online).
Waanzilishi wa mradi huo Nissan Bahar na Franky Imbesi wamefaulu kupata ufadhili wa dola milioni kumi kutoka kwa wawekezaji wa Japan zitakazotumika kuzindua sarafu hiyo ya dijitali na pia kutengeneza benki ya kuthibitisha hatua na uhamisho wowote wa fedha
Nchi ambazo kwa Upande wa Afrika zitakuwa ni Kenya na Malawi na Sehemu zingine itakuwa ni Japan na Uingereza.
Ukiangazia kwa upande wa Afrika, mradi huo utasaidia sana kuongeza Vipato kwa wa Afrika kwa kuwa huwa wanatumia mda mwingi kutembea kuelekea mashuleni, kazini na sehemu za biashara.
KIFAA HICHO KITAFANYAJE KAZI?
Ili kuweza kutambua umbali unaotembea ni lazima uwe umeweka plogramu hiyo kwenye simu yako na kuvaa kifaa katika mkono wako ambao kitafanya kuhesabu hatua zako kwa umakini zaidi.
0 comments:
Post a Comment