UNAFAHAMU KUWA VLC INAWEZA CONVERT VIDEO ZAKO?

Kupitia mtandao wa habari wa teknology, Teknokona umeleeza kuwa programu ya VLC ambayo inatumika karibia na watu wengi Duniani ina uwezo wa kubadilisha(Convert) Video zako kwenda katika mifumo mingine.


Hizi ndizo hatua ambazo zinaweza kubadilisha Video yako kuwa katika mfumo wa mp4, mp3 na mifumo mingine.

1:HATUA YA KWANZA
Fungua Programu yako ya Vlc kwenye computer yako, kisha elekeza mouse yako mpaka kwenye sehemu ya media, bonyeza hapo kisha bonyeza tena kwenye Convert/save....
convert save
2:HATUA YA PILI
Hatua inayofuata ni kuweka hilo file ambalo unataka kulibadilisha ambapo utaona sehemu kumeandikwa add na sehemu ya chini ni kama ukiamua kuweka subtitle kwenye hilo file ambalo unaitaji kulibadilisha.
open file

3:HATUA YA TATU
Baada ya kumaliza hatua ya tatu ya kuweka file ambalo unataka uli convert, sasa bonyeza kwenye convert, ukishamaliza chagua mahala ambapo unataka hilo file ulilolibadilisha lipatikane sehemu gani na manisha Destination. Eneo hilo la kubadilisha mahala ambapo utakuta hilo file ni hapo palipowekewa alama nyeusi kwenye Browse, baada ya hapo unabonyeza Start kisha file lako linaanza kubadilishwa.
destination file

Kulingana na ukubwa wa File lako mchakato huo unaweza ukatumia muda mrefu au muda mchache tu.

SOURCE: TEKNOKONA

0 comments:

Post a Comment