Mji mmoja kaskazini mwa Iceland umekuwa kipeperusha bendera ya taifa nusu mlingoti kila mkazi wa mji huo anapofariki.
Lakini sasa, madiwani wa mji huo wa Husavik wenye wakazi 2,000 wameamua kusitisha utamaduni huo.
Wanasema utamaduni huo sasa haufai kwa sababu wakazi hawajuani kama ilivyokuwa zamani, na si lazima wakazi wawe wanamfahamu aliyefariki, haya kwa mujibu wa gazeti la Morgunbladid.
Husavik huvutia sana watu wanaofika kutazama nyangumi na diwani mmoja kutoka eneo hilo Hjalmar Bogi Haflidason anasema kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti huwa kunashangaza watalii.
“Wengi huwa wanadhani kiongozi wa nchi amefariki,” anasema.
Uamuzi huo haukupitishwa kwa kauli moja, na kumbukumbu za mkutano zilizopakiwa mtandaoni zinaonyesha kuna madiwani kadha waliopinga mpango huo.
Mmoja wao Sofia Helgasdottir aliambia tovuti ya Visir kuwa: "Huu ni utamaduni ulioanza zamani na tumekua nao. Ninafikiri ni utamaduni mzuri sana.”
Kuhusu wageni kushangazwa, amesema wageni hao ndio wanaofaa kujifunza tamaduni za wenyeji.
SOURCE:BBC
0 comments:
Post a Comment