Shrikisho la soka la Uingereza FA limempa adhabu Jose Mourinho kwa utovu wa nidhamu alipokuwa uwanjani kwenye mechi dhidi ya West ham United.
Mourinho amefungiwa mechi moja na faini ya pound 40,000 baada ya kukiri mwenyewe kuwa alitumia lugha isiyokubalika uwanjani baada ya timu yake ya Chelsea kufungwa na timu ya West ham mwezi uliopita tarehe 24.
Na wiki hii anatarajia kupokea barua ya sababu ya adhabu zake ambazo amekiri mwenyewe kufanya na hiyo pia itamfanya Morinho kukosa mechi ya ligi siku ya Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment