HAYA NDIYO MANENO YA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU KUTOSHIKA SIMU YA MPENZI WAKE ZARI

Kushika simu ya mwenza wako ni kitu ambacho kinaweza leta ugomvi ndani ya nyumba hata kwenye mahusiano.
Kupitia Mahojiano yaliyofanywa na Millard Ayo, Diamond platnumz amesema kuwa hawez pakua kabisa simu ya mpenzi wake Zari.

Simu za Mkononi zimevunja mahusiano ya wapenzi wengi ambao wanapenda kwa dhati, 

Diamond na Zari wote ni watu maarufu na wanamashabiki wengi ambao kila mmoja wao anapendwa na mashabiki na kuhitaji kuwa nao karibu zaidi, na hii ndio sababu ambayo Diamond ameona kumwamini mpenzi wake Zari bila ya kupekua Simu yake.


"Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa" Jibu la Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama anashika simu ya mpenzi wake Zari.

"Sidiriki kwasababu namjua ni binadamu, ukizingatia na yeye ni mtu maarufu, so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, smtmes anaweza mjibu mtu akamwitikia poa, kwangu mimi kitanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo sitaki kabisa kugusa simu yake"

"Simu yangu mimi haina password naiachaga tu lakini naye pia hagusagi simu yangu kabisa kwasababu simu zinaleta ugomvi mwingi" Aliendelea kusema Diamond.

Diamond pia alitoa ushauri wa bure kwa watu wengine ambao wanapenda shika simu za wapenzi wao

"Simshauri mtu kushika simu ya mpenzi wake, cha muhimu ni kuzingatia kama anakupenda, anakujali na anakuthamini na umuone na hivyo vitu lakini katika simu mwache chochote anachojua yeye" Alimaliza Diamond.

0 comments:

Post a Comment