Joseph haule a.k.a professor Jay amechaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi
mkoani Morogoro kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kuwangusha wapinzani wake vikali.
Kwa mujibu wa Luninga ya ITV, msimamizi wa jimbo la mikumi alimtangaza rapper huyo Professor Jay kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo kwa kuwa na Kura 32,259 akiwaacha wapinzani wake kwa tofauti ya Kura 1834, Mgombea wa tiketi ya CCM ambaye ndiye alikuwa mpinzani mkubwa kwake Jonas Nkya alipata kura 30,425.
Joseph Haule anakuwa Rapper wa pili kuingia Bungeni baada ya Joseph sugu Mbilinyi kuwa naye Mbunge wa Mbeya mjini kwa mara ya pili
0 comments:
Post a Comment