PAUL WALKER AINGIA KWENYE ORODHA YA MATAJIRI MAREHEMU

Mwigizaji nyota wa Fast & Furious Paul Walker ameingia kwenye orodha ya karibuni zaidi ya Forbes ya wasanii marehemu wanaopata pesa nyingi zaidi.

Walker, aliyefariki katika ajali ya barabarani 2013, alijizolea $10.5m (£6.8m) mwaka mmoja uliopita na sasa yumo katika nambari tisa.

Michael Jackson anaongoza kwa mwaka wa tatu mtawalia, akipokea $115m (£75m), ingawa ameshuka kutoka $140m alizojizolea 2014.

Elvis Presley yumo nambari ya tatu $55m (£35.8m), naye aliyetunga filamu ya Peanuts creator Charles Schulz yumo nambari nne na $40m (£26m).

Hawa hapa ndio wasanii 13 walio kwenye orodha hiyo ya Forbes:

Michael Jackson: $115m (£75m)Elvis Presley: $55m (£35.8m)Charles Schulz: $40m (£26m)Bob Marley: $21m (£13.7m)Elizabeth Taylor: $20m (£13m)Marilyn Monroe: $17m (£11m)John Lennon: $12m (£7.8m)Albert Einstein: $11m (£7.1m)Paul Walker: $10.5m (£6.8m)Bettie Page: $10m (£6.5m)Theodor Geisel (Dr Seuss): $9.5m (£6.1m)Steve McQueen: $9m (£5.8m)James Dean: $8.5m (£5.5m)

0 comments:

Post a Comment