NGUZO TANO MUHIMU ZA BREAK DANCE

Una kipaji cha Breakdance ila haujui uanzie wapi, Hizi ni nguzo tano za kuzifuata kama kweli unahitaji kuwa Breakdancer(Bboy,Bgirl) mzuri na kuweza kuchukua mataji katika mashindano tofauti iwe ya Dance 100% au mtaani unashindana na jamaa.


1.TOP ROCKS
Aina hii huwa inamsaidia Bboy kuuweka mwili katika hali ya ushindani zaidi na inakufanya mwili unakuwa tiyari kuonesha miondoko tofauti tofauti na ndio maana Bboy mzuri lazima ujue jinsi gani ya kuandaa mwili.
Hata kama hufahamu ku Breaking ila ukianza na vionjo hivi tiyari umeshatengeneza hisisa kwa mashabiki wanaokutizama kuona kua unaweza Breakdance.


2.FLLOR ROCKS
Floor rocks ni style ambayo sasa inakuwa inawaonyesha majaji na watazamaji kwamba uko tiyari kucheza na kuonesha style tofauti, kama ilivyo Toprocks lakini huku kwenye Floor rocks, mikono inakuwa imegusa sakafu.



3.POWER MOVES
Hapa sasa ndipo Bboy anachukua kura nyingi kutoka kwa majaji kwasababu powermoves ni style ambazo zinaitaji mazoezi ya marakwamara na ndio maana Breakdance wengi ambao hawafamu nguzo hizi huwa anakimbiria sana huku kwenye powermove kujikombea kura nyingi lakini Breakdance mzuri lazima ujue kuanza na juu mpka chini



4. SUICIDES
Ukiachia mbali Power moves, kitu kingine ambacho unaweza waacha midomo wazi majaji na mashabiki ni Suicide, ni staili ambayo inaitaji mazoezi ambayo yanazidi hata mwaka au miezi kutokana na kuwa ngumu mno.

Kama ndio kwanza unaanza Breakdance hauruhusiwi kutumia staili hii kwani baadhi ya ma Dancer ambao walijaribu staili hii walivunja baadhi ya viungo vyao.



5.FREEZES
Hii ndio staili ya mwisho pale unapokuwa unamalizia round yako ya Breakdance, sasa huwezi kumaliza bila kuweka mbwembwe ili kuonesha kuwa bado mwili haujochoka.

Ili kuweza kumudu staili ya Freze lazima uwe na mazoezi ya yoga ili kuweka viungo vyako vizuri kwani staili hii huwa inakuwa na maumbo tofauti ambayo unaweza kumshawishi jaji kukupa maksi nyingi zaidi kwenye shindano lako.



Hizo ndizo nguzo tano na zamsingi pale unapokuwa katika shindano la ku Breakdance kwani ukianza na nguzo ya kwanza mpka ya mwisho lazima uonekana kweli we ni mtaalamu wa miondoko ya Breakdance.

0 comments:

Post a Comment