Mashindano ya kudance ya Dnce 100% hatua ya fainali itafanyika leo katika viwanja vya Don bosco Upanga jijini Dar es salaam, ambapo mashindano haya yataanza majira ya mchana, huku mshindi w kwanza ataondoka na kitita cha shilingi milioni 5, kutoka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo ambao ni Vodacom Tanzania, pia shindano hilo litakuwa chini ya wandalizi wa shindano hilo ambao ni EATV.
Makundi ambayo yameingia hatua ya fainali na yanatarajia kupambana leo ni Team makorokocho, Best boyz kaka zao, The winners crew, Team ya shamba na The W.D.
Wote hawa wataoneshana jinsi ya kudance kwa staili tofauti ambazo zitawapelekea mmoja wapo kuibuka kidedea wa Dance 100% 2015.
Matina Nkurlu Meneja uhusiano kutoka Vodacom, yeye alizungumza kwa kuwataka wasanii wetu wa Bongo kuja kwa wingi ili kutoa sapoti na kuangalia kundi moja ambalo wanaweza fanya nalo kazi.siku za mbeleni.
0 comments:
Post a Comment