Baada ya tetesi nyingi sana kusambaa kuhusu mpenzi wa zamani wa Ciara, Future na aliyewahi kuwa mpenzi wa zamani wa Tyga,Blac Chyna kuwa ni wapenzi, sasa hivi inaonekana wazi kuwa mmoja wao hana chochote cha kuficha juu ya hisia alizonazo kwa mwenzake!
Blac Chyna ambaye aliachana na Tyga mwaka 2014, ameingia kwenye headlines baada ya kaamua kuhalalisha tetesi zote zinazosambaa mitandanoni juu yake na Future kwa kuchoratattoo mpya mkononi ya jina la rapper huyo.
Ukaribu wa mastaa hawa wawili ulianza kuweka headlines kubwa sana baada ya camera kuwanasa wawili hao wakiondoka pamoja kwenye club moja yenye jina D.C Clubna licha ya wawili hao kutokusema chocote juu ya ukaribu wao toka siku hiyo, tattoo mpya yaBlac Chyna inaonekana kujibu tetesi nyingi zilizokuwa zinasambaa kwenye websites na mitandao mbalimbali ya kijamii
0 comments:
Post a Comment